Mwenyekiti wa Yanga,Yussuf Manji amefanikiwa kutetea nafasi yake katika uchaguzi uliofanyika Jumamosi usiku katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Manji ambaye hakuwa na mpinzani katika uchaguzi huo ameshinda kwa kupata kura 1468 huku kura mbili pekee zikiharibika.
Nafasi ya Makamu Mwenyeki imeenda kwa Clement Sanga aliyepata kura 1428 dhidi ya kura 80 za mpinzani wake Tito Osoro.
Nafasi nyingine iliyogombewa ni Ujumbe ambapo wajumbe wanane wamepatikana.
SAFU KAMILI YA UONGOZI WA YANGA SC
WENYEVITI
1. Yussuf Mehboob Manji M/KITI
2. Clement Sanga MAKAMU M/ KITI
WAJUMBE
1. Omary Ameir
2. Siza Lyimo
3. Salum Mkemi
4. Thobius Lingalangala
5. Ayoub Nyenzi
6. Samwel Lukumay
7. Hashim Abdallah
8. Hussein Mnyika
0 comments:
Post a Comment