728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 12, 2016

    YANGA SC YAWAENDEA UTURUKI MO BEJAIA BILA YA NYOTA WAKE WATANO

    Dar es Salaam,Tanzania.

    MABINGWA wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na wawakirikishi pekee wa michuano ya kimataifa toka ukanda wa Cecafa,Yanga SC wameondoka nchini leo alfajiri wakiwa na kikosi cha wachezaji 22 kuelekea Uturuki ambako wataweka kambi ya muda mfupi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wake wa kwanza wa kundi A wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria Juni 17/18 huko Bejaia,Algeria.

    Katika msafara/kikosi hicho Yanga SC imewaacha nyota wake watano kwa sababu mbalimbali.Juma Abdul na Malimi Busungu wameachwa kwa kuwa ni majeruhi,Mlinda mlango Benedictor Tinocco na mshambuliaji Paul Nonga wao wameachwa kutokana na kutokuwa katika programu ya mwalimu.

    Mwingine aliyeachwa ni Salum Telele.Telela ameachwa kwa sababu amemaliza mkataba wake na majaaliwa ya kurejea kwake kikosini yatategemea iwapo atapewa mkataba mpya.

    Mtogo Vincent Bossou yeye anatarajiwa kuungana na wenzake huko Uturuki akitokea nyumbani kwao Togo alikokwenda kwa sababu za kifamilia.

    KIKOSI KILICHOONDOKA

    Makipa:Ally Mustafa ‘Barthez’, Deo Munishi ‘Dida’ na Benno Kakolanya.

    Mabeki; Hassan Kessy, Mwinyi Haji,Oscar Joshua, Andrew Vincent ‘Dante’, Mbuyu Twite, Kevin Yondan,Pato Ngonyani na Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro'.

    Viungo; Thabani Kamusoko, Juma Mahadhi, Said Juma ‘Makapu’,Simon Msuva, Haruna Niyonzima,Deus Kaseke na Godfrey Mwashiuya.

    Washambuliaji; Donald Ngoma,Matheo Anthony na Amissi Tambwe.

    BENCHI LA UFUNDI

    Hans van der Pluijm -Kocha Mkuu, Juma Mwambusi-Kocha Msaidizi Juma Pondamali -Kocha wa makipa, Edward Bavu -Daktari ,Jacob Onyango- Mchua Misuli,Mohammed Mpogolo-Mtunza Vifaa na Hafidh Saleh -Meneja


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: YANGA SC YAWAENDEA UTURUKI MO BEJAIA BILA YA NYOTA WAKE WATANO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top