728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 12, 2016

    COPA AMERICA CENTENARIO:COLOMBIA HOI KWA COSTA RICA YACHAPWA 3-2 YASHUKA MPAKA NAFASI YA PILI KUNDI A

    Houston, Marekani.

    COLOMBIA imeshindwa kubaki kileleni mwa Kundi A la hatua ya makundi ya michuano ya Copa America Centenario baada ya alfajiri ya leo kufungwa mabao 3-2 na Costa Rica katika mchezo mkali uliochezwa katika uwanja wa NRG, Houston.

    Mabao ya Costa Rica yamefungwa na John Venegas,Celso Borges na Frank Fabra aliyejifunga huku yale ya Colombia yakifungwa na Frank Fabra na Marlos Moreno.

    Msimamo wa Kundi A uko kama ifuatavyo:

    1. Marekani - 6
    2. Colombia - 6
    3. Costa Rica - 4
    4. Paraguay - 1

    VIKOSI

    Colombia: Róbinson Zapata - Stefan Medina,Yerry Mina, Felipe Aguilar, Frank Fabra -Carlos Sánchez, Guillermo Celis, Sebastián Pérez, Dayro Moreno - Marlos Moreno,Roger Martínez. 

    Costa Rica: Patrick Pemberton - Johnny
    Acosta, José Salvatierra, Kendal Watson,Francisco Calvo - Ronald Matarrita, Celso Borges, Christian Bolaños, Randall Azofeifa,Bryan Ruiz - Johan Venegas. 

    Katika mchezo wa mapema wenyeji Marekani waliifunga Paraguay 1-0 na kufuzu robo fainali.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: COPA AMERICA CENTENARIO:COLOMBIA HOI KWA COSTA RICA YACHAPWA 3-2 YASHUKA MPAKA NAFASI YA PILI KUNDI A Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top