Santa Clara,Marekani.
Wenyeji timu ya taifa ya Marekani wameianza vibaya michuano ya Copa America Centenario baada ya alfajiri ya leo kukubali kichapo cha mabao 2-0 toka kwa timu ya taifa ya Colombia katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi A uliochezwa katika uwanja wa Levi's Stadium,Santa Clara.
Mabao yaliyoipa ushindi huo muhimu Colombia yamefungwa dakika za 8 na 42 kupitia kwa mlinzi wake Christian Zapata na mshambuliaji wake James Rodriguez..
Rodriguez alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penati uliotolewa na mwamuzi Roberto Garcia baada ya mlinzi wa Marekani DeAndre Yedlin kushika mpira ndani ya boksi.
0 comments:
Post a Comment