Hampshire,England
Shabiki Luke Bryant, 25,mkazi wa Bankhill Drive, Lymington,
Hampshire ambaye siku ya mwaka mpya alizua kizaa zaa baada ya kujipenyeza na hatimaye kumvaa kocha Arsene Wenger katika dimba la St Mary's huenda akakumbwa na adhabu kali siku chache zijazo kufuatia sakata lake kufikishwa mahakamani.
Bryant alishindwa kuzuia hasira zake na kuamua kutoka jukwaani alikokuwa amekaa na kwenda katika benchi la ufundi la klabu ya Arsenal na kumtolea maneno makali kocha Arsenal Wenger kabla ya polisi waliokuwa uwanjani hapo kuwahi na kumtia nguvuni.
Shabiki huyo alifikia uamuzi huo baada ya kukerwa na soka bovu lililokuwa likionyeshwa na Arsenal na kupelekea timu hiyo ya London kuambulia kipigo cha magoli 2-0 toka kwa wenyeji Southampton katika muendelezo wa mechi za Epl.
Bryant atapanda kizimbani januari 22 mwaka huu huko Southampton kujibu tuhuma hiyo ambayo inakwenda Kinyume na sheria ya mwaka 1991 inayozuia mashabiki au mtu yoyote asiye husika kuingia eneo la mchezo wakati mchezo ukiendelea.
0 comments:
Post a Comment