Makala na Paul Manjale
Pengine mnaweza kujiuliza huyu mtu ni nani na kwanini namuita ni kiboko ya Pele.....pata mchapo kamili.
Anaitwa Arthur Friedenreich mchezaji wa kwanza mweusi wa kulipwa kutokana na wakati
huo soka kuwa ni mchezo wa wazungu pekee....Arthur alizaliwa tarehe 18 July 1892 katika jiji la Sao Paulo nchini Brazil toka kwa
baba mjerumani na mama mweusi Mathilde mtoto wa mtumwa.
Alianza kucheza soka akiwa na klabu ya Sc Germania kwa ushawishi wa baba yake(timu
hiyo ilikuwa inaundwa na idadi kubwa ya wajerumani waliokuwa wakiishi Sao Paulo).
Klabu alizochezea:Sc Germania,Sao Paulo,Atletico Mineiro na Flamengo.
KIOJA:
Atoswa timu ya taifa iliyoshiriki kombe la dunia mwaka 1930 Uruguayi.
KISA??
Kabla ya michuano hiyo kulikuwa na mgogoro kati ya ligi za majimbo ya Sao Paulo na Rio de
Janeiro.Kutokana na mgogoro huo wachezaji kutoka Rio de Janeiro pekee ndiyo walio safiri
kwenda Uruguayi kushiriki kombe la dunia huku Arthur aliyekuwa na miaka 38 na wakali wengine kama Filo na Feitico wakikosa safari hiyo.
Mpaka anastaafu soka mwaka 1935 alikuwa na rekodi ya kufunga mabao 1329 katika michezo 1239 huku mashabiki wa Pele wakipinga rekodi hiyo na kusema Arthur alifunga mabao 1239 katika michezo 1329.....kinachowapa kiburi mashabiki wa Pele ni kwamba uhifadhi mbaya wa kumbukumbu ndiyo ulikwamisha rekodi hii
kukubarika FIFA......Pele ana rekodi ya goli
1281-1363 michezo...
0 comments:
Post a Comment