728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, May 11, 2017

    Singida United yamnasa Batambuze wa Tusker ya Kenya


    Nairobi,Kenya.

    BEKI wa kushoto wa kimataifa wa Uganda na Tusker ya Kenya,Shafik Batambuze amesaini kandarasi ya awali ya miaka miwili ya kujiunga na Singida United ya mkoani Singida.

    Habari ambazo Soka Extra imezipata zinasema Batambuze mwenye umri wa miaka 22 ameingia kandarasi hiyo jana Jumatano jijini Nairobi,Kenya baada ya kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na Mkurugenzi wa Singida United,Festo Sanga.

    Batambuze alitua ligi kuu ya soka ya Kenya mwaka 2012 na kujiunga na klabu ya Muthoroni Youth akitokea Simba ya nyumbani kwao Uganda.Pia alivichezea vilabu vya Western Stima na Sofapaka kabla ya kujiunga na Tusker.

    Mwaka jana Batambuze aliisaidia Tusker iliyokuwa ikinolewa na Mganda,Paul Nkata kushinda ubingwa wa ligi kuu ya Kenya na kumaliza ufalme wa miaka mitatu wa Gor Mahia.

    Mafaniko hayo yalimpa Batambuze nafasi ya kuiwakilisha Uganda kwenye michuano ya AFCON iliyofanyika Januari mwaka huu huko nchini Gabon.

    Batambuze anakuwa mchezaji wa nne kujiunga na Singida United baada ya Wazimbabwe,Elisha Muroiwa,Wisdom Mtasa na Twafaza Kutinyu.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Singida United yamnasa Batambuze wa Tusker ya Kenya Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top