728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 12, 2017

    Manchester,Ajax zafuzu fainali Europa Ligi


    Manchester,England

    Manchester United na Ajax zimefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Europa Ligi baada ya Alhamisi usiku kuziondosha mashindanoni timu za Celta Vigo na Lyon kwenye michezo ya marudiano ya hatua ya nusu fainali.

    Manchester United ikiwa nyumbani Old Trafford imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Celta Vigo.Manchester United ilipata bao lake kupitia kwa Marouane Fellaini aliyefunga kwa kichwa kabla ya Facundo Roncaglia kuifungia Celta Vigo bao la kusawazisha.

    Aidha katika mchezo huo ilishuhudiwa timu hizo zikimaliza pungufu baada ya nyota wao wawili Eric Bailly na Roncaglia kutolewa nje kwa kadi nyekundu na mwamuzi Ovidiu Alin Hategan kwa mchezo usio wa kiungwana.

    Manchester United imefuzu finali kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1.Ikumbukwe Manchester United ilishinda bao 1-0 kwenye mchezo Wa awali. 

    Katika mchezo mwingine Ajax imefuzu fainali licha ya kufungwa mabao 3-1 na Lyon kwa mabao ya Alexandre Lacazette aliyefunga mara mbili na Rachid Ghezzal.Bao la Ajax limefungwa na Kasper Dolberg.


    Ikumbwe katika mchezo wa awali uliochezwa Jumatano iliyopita huko Amsterdam,Ajax iliifunga Lyon mabao 4-1 hivyo inafuzu fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-4.

    Fainali ya michuano ya Europa itachezwa Stockholm, ,Sweden Jumatano Mei 24 mwaka huu ambapo timu itakayoshinda itapata zawadi ya kikombe pamoja na kupewa nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya msimu ujao.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Manchester,Ajax zafuzu fainali Europa Ligi Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top