Baada ya kiungo Jonas Mkude kurejea kimya kimya nchini akitokea Afrika Kusini kufanya majaribio katika klabu ya Bidvest Wits mambo mengi yamesemwa kuhusiana na safari hiyo.
Wapo waliosema Mkude amefeli huku wengine w
akisema amefaulu hivyo basi kutokana na mkanganyiko huo mwenyekiti wa Kamati ya Usajil ya Simba, Zacharia Hans Poppe ameweka hadharani ukweli wa mambo.
Poppe amesema
“Mkude siyo kwamba ametoswa mo kwa moja kule Wits isipokuwa wamesema walikuwa na wachezaji wengi wa majaribio, hivyo yeye (Mkude) amerejea nchini kisha wataendelea kumfanyia tathmini kina katika ligi ya nyumbani.
“Wametoa miezi mitatu ya kumchunguza kisha baada ya hap watakuwa na kitu cha kutuambia kama wameridhika naye au la.
0 comments:
Post a Comment