Barcelona,Hispania.
STAA wa Barcelona na Argentina,Lionel Messi Juni 30 ya mwaka huu atafunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi mrembo,Antonello Roccuzzo .
Ndoa hiyo inayotarajiwa kuvuta hisia za watu wengi kutokana na umaarufu wa wapenzi hao itafungwa huko Arroyo Seco,Rosario, kaskazini mashariki mwa nchi ya Argentina ambako ni nyumbani kwa wawili hao.
Taarifa kutoka nchini Argentina zinasema ndoa hiyo itasherekewa kwa muda wa siku sita ikianzia Rosario na kuishia jijini Barcelona kwenye mgahawa wa 9 Reinas ambapo wageni waalikwa zaidi ya 600 wanatarajiwa kuhudhuria.
Messi na Roccuzzo wamekuwa wapenzi kwa kipindi cha miaka na wamebarikiwa kupata watoto wawili wa kiume Thiago mwenye umri wa miaka minne na Mateo mwenye umri wa miaka miwili.
Mapenzi kati ya wawili hao yalianza mwaka 2008 baada ya kukutanishwa na Lucas Scaglia ambaye ni rafiki wa karibu wa Messi na binamu wa Roccuzzo.
0 comments:
Post a Comment