728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 16, 2017

    Schmeichel,Ndidi watamba usiku wa tuzo Leicester City


    Leceister,England.

    USIKI wa Jana Jumatatu Leicester City walikuwa na kazi moja tu,kuwatunuku kwa tuzo wachezaji wao waliofanya vizuri klabuni hapo kwa msimu wa mwaka 2016/17 katika hafla iliyofanyika huko King Power.

    Katika hafla hiyo imeshuhudiwa Mlinda Mlango namba moja wa klabu hiyo,Kasper Schmeichel akiibuka kidedea baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo mbili za mchezaji bora wa msimu chaguo la klabu na mashabiki baada ya kupata kura zaidi ya asilimia 75 zilizopigwa kupitia mitandao. 

    Schmeichel,30,ametwaa tuzo hizo baada ya msimu huu kuonyesha kiwango bora kilichoisaidia Leceister City kufika robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Ulaya.Katika michuano hiyo alifungwa mabao matatu tu katika michezi minane huku katika michezo minne ya kwa akicheza bila kuruhusu bao.




    Tuzo ya mchezaji bora chipukizi imekwenda kwa Mnigeria,Wilfred Ndidi wakati tuzo ya bao bora la msimu ikienda kwa kiungo wa England,Danny Drinkwater.



    Tuzo ya mchezaji bora wa Akademi imekwenda kwa mlinzi,Alex Pascanu ambaye amekuwa mhimili mkubwa kwenye vikosi vya U-18 na U-23 vya klabu hiyo.Harvey Barnes ametwaa tuzo ya mchezaji aliyeonyesha mafanikio maarufu kama Development Squad Player of the Season Award.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Schmeichel,Ndidi watamba usiku wa tuzo Leicester City Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top