728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 16, 2017

    AFCON:Kundi la Serengeti Boys lazidi kuwa gumu,Angola,Niger nazo zatoka sare


    Libreville,Gabon.

    YACINE Wa Massamba wa Niger akiwania mpira na Adalmiro Patricio Pacheco Da Silva wa Angola kwenye mchezo wa pili wa kundi B wa kuwania ubingwa wa michuano ya AFCON ya U-17 uliochezwa Jumatatu Usiku na kumalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2 huko Stade de L’amitie d’Angondje,Libreville, Gabon ambapo Tanzania inawakilishwa na Serengeti Boys.

    Niger ndiyo walioonekana kama wangeibuka na ushindi kwenye mchezo huo baada ya muda mrefu kuongoza kwa mabao mawili ya Abdoul Karim ya dakika za 27' na 42' lakini ghafla Angola waliamka na kusawazisha mabao hayo kupitia kwa Muondo Melono 67' na Joao Jelson 82'.

    Sare hiyo imezifanya Angola na Niger zijikite kileleni mwa kundi B zikiziacha nyumba Mali na Tanzania ambazo katika mchezo wa kwanza zilitoka sare tasa ya bila kufungana.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: AFCON:Kundi la Serengeti Boys lazidi kuwa gumu,Angola,Niger nazo zatoka sare Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top