728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, May 16, 2017

    Cavani mchezaji bora Ufaransa,Mbappe chipukizi bora,N'Golo Kante,Depay nao wakomba tuzo


    Paris,Ufaransa.

    MSHAMBULIAJI wa Paris Saint-Germain,Edinson Cavani (Pichani) akitabasamu baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa maarufu kama Ligue 1 katika hafla iliyofanyika Jumatatu usiku.

    Cavani,30,ametwaa tuzo hiyo baada ya msimu huu kuifungia Paris Saint-Germain mabao 48 kwenye michuano yote.Mabao 35 yakiwa ni ya Ligue 1 na kuwa karibu kuvunja rekodi ya mabao 50 iliyowekwa msimu uliopita na Zlatan Ibrahimovic.

    Nafasi ya pili imechukuliwa na Bernardo Silva wa AS Monaco huku nafasi ya tatu ikienda kwa Alexandre Lacazette wa Lyon.Tuzo ya mchezaji bora wa kike imekwenda kwa Sakina Karchaoui wa Montpellier.


    Staa wa AS Monaco,Kylian Mbappe ametangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora chipukizi baada ya msimu huu kufunga mabao 14 na kupika mengine 11.Ikumbukwe Mbappe,18,amekuwa ni mhimili kubwa kwa AS Monaco akiisaidia timu hiyo kufika nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa Ulaya na kuongoza Ligue 1.

    Tuzo ya kocha bora wa msimu imekwenda kwa Leonardo Jardim wa AS Monaco huku tuzo ya kipa bora ikienda kwa Danijel Subasic pia wa AS Monaco. 

    Kiungo wa Chelsea,N'Golo Kante amechaguliwa mchezaji bora wa msimu wa Ufaransa kwa wachezaji wanaocheza nje.Msimu uliopita tuzo hiyo ilikwenda kwa Antoine Griezmann.

    Tuzo ya bao bora la msimu imeenda kwa winga wa zamani wa Manchester United,Memphis Depay ambaye kwa sasa anaichezea Lyon.

    Kikosi bora cha Msimu (4-3-3): Danijel Subasic (Monaco); Djibril Sidibe (Monaco), Kamil Glik (Monaco), Thiago Silva (PSG); Benjamin Mendy (Monaco), Jean-Michael Seri (Nice),Marco Verratti (PSG), Bernardo Silva(Monaco); Alexandre Lacazette (Lyon),Edinson Cavani (PSG), Kylian Mbappe (Monaco)

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Cavani mchezaji bora Ufaransa,Mbappe chipukizi bora,N'Golo Kante,Depay nao wakomba tuzo Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top