728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, May 15, 2017

    Deal Done:Arsenal yamnasa Sead Kolasinac,yampa mshahara mnono


    London, England.

    ARSENAL imeanza mapema ujenzi wa kikosi chake tayari kwa msimu ujao wa ligi kuu ya soka nchini England hii ni baada ya leo mchana kuripotiwa kukamikisha usajili wa beki wa kushoto wa kimataifa wa Bosnia,Sead Kolasinac anayekipiga Shalke 04 ya Ujerumani.

    Taarifa kutoka Sky Sports zinasema Kolasinac mwenye umri wa miaka 23,anayetumia vyema mguu wa kushoto na mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani atajiunga na Arsenal Julai 1 pindi mkataba wake na Shalke 04 utakapofikia mwisho Juni 30 mwaka huu.

    Kolasinac amesaini mkataba wa miaka mitano na atakuwa akilipwa mshahara wa £120,000 kwa wiki na kuwa mchezaji wa tatu anayevuta mkwanja mrefu zaidi baada ya Mesut Ozil anayelipwa £140,000 na Alexis Sanchez anayelipwa £130,000.


                                                 


    Ujio wa Kolasinac kwenye kikosi cha Arsenal umeanza kuibua maswali juu ya hatima ya mabeki Nacho Monreal na Kieran Gibbs ambao wameshindwa kuonyesha kuyamudu vyema majukumu yao uwanjani.

    Kolasinac anaiacha Shalke 04 akiwa ameichezea zaidi ya michezo 115.Msimu huu Kolasinac ameifungia timu hiyo mabao matatu na kupika/kutengeneza tisa katika michezo 39.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Deal Done:Arsenal yamnasa Sead Kolasinac,yampa mshahara mnono Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top