Dar Es Salaam,Tanzania.
KADI nyekundu ya mshambuliaji wa Kagera Sugar Mbarak Yusufu imefutwa na sasa yupo huru kucheza mechi ya mwisho dhidi ya Azam FC Mei 20, 2017.
Uamuzi huo umefikiwa katika kikao kilichokaa jana na kupitia taarifa mbalimbali za michezo iliyochezwa, ambapo kamati ilijiridhisha kuwa mwamuzi alimpa kimakosa kadi nyekundu mshambuliaji huyo.
Wakati Mbaraka akiruhusiwa kucheza mchezo ujao, mwamuzi aliyechezesha mchezo kati ya Yanga dhidi ya Kagera Sugar ,Ngole Mwangole ameondoshwa kwenye orodha ya waamuzi wa ligi kuu.
Ngole Mwangole mwamuzi bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, alimuonyesha kadi nyekundu ya moja kwa moja Mbaraka Yusuph katika mchezo ulioishia kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2- 1.
0 comments:
Post a Comment