Dar Es Salaam,Tanzania.
BAADA ya jana mwenyekiti wa kamati ya usajili wa SImba SC, Zakaria Hans Pope kutangaza kujiuzulu, leo asubuhi taarifa zinaeleza kuwa Pope ameamua kubadili maamuzi yake na kurejea katika kamati hiyo.
Uamuzi wa Hans Poppe kurejea Simba umetokana na mkutano unaoelezwa kufanyika jana mpaka saa 9 usiku wa kuamkia leo.
Hans Poppe amethibitisha mwenyewe kurejea kwake kundini baada ya mkutano huo na viongozi.
Hans Poppe aliamua kujiondoa katika kamati ya utendaji ya Simba na akawa ametoka moja kwa moja kwenye kamati ya usajili aliyokuwa mwenyekiti.
“Kweli tumekutana hadi saa 9 usiku, mwisho tumekubaliana na tumeyamaliza vizuri. Huu ni wakati wa kusonga mbele,” alisema Hans Poppe.
0 comments:
Post a Comment