728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 10, 2017

    Messi Haombi Jezi Lakini Ukimpa Haitupi


    Barcelona,Hispania.

    BAADA ya wiki iliyopita kudai kuwa huwa hana tabia ya kuomba omba jezi kwa wachezaji wa timu pinzani labda wao ndio wamuombe ama wawe ni raia wenzake wa Argentina,staa wa Barcelona Lionel Messi ameonyesha kwamba inapotokea kapewa jezi na mtu huwa haitupi na badala yake anaiweka kwenye chumba chake maalumu cha kumbukumbu.

    Baadhi ya nyota ambao jezi zao zimeonekana kwenye chumba cha makumbusho cha Messi ni pamoja za jezi za nyota wa zamani wa Real Madrid Raul Gonzalez Blanco, Deco De Souza, Thierry Henry, Pavel Nedved.

    Wengine ni Philipp Lahm, Iker Casillas,Francesco Totti,Gerard Pique,Luis Suarez na nyota wa Westham United,Michael Lanzini ambaye kwa mujibu wake amesema hajawahi kucheza dhidi ya Messi lakini walipeanza jezi baada ya kukutana jijini Barcelona alikokuwa amekwenda kupatiwa matibabu ya goti.

    Hivi karibuni Messi alifichua kwamba hajawahi kuomba jezi kwa wachezaji wa timu pinzani ila aliwahi kuomba mara moja tu kwa Zinedine Zidane ambaye kwa sasa ni kocha wa Real Madrid na kuongeza kuwa wengi huwa anabadilishana nao tu baada ya wao kumuomba.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Messi Haombi Jezi Lakini Ukimpa Haitupi Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top