728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 10, 2017

    Sadio Mane mchezaji bora wa mwaka Liverpool,Can,Leiva wachomoka na tuzo


    Liverpool,England.

    WINGA wa kimataifa wa Senegal,Sadio Mane usiku wa kuamkia leo Jumatano ameibuka kidedea baada ya kutangazwa mshindi mara mbili wa kinyang'anyiro cha kumsaka mchezaji bora wa mwaka wa Liverpol kwa msimu wa 2016/17 katika hafla ilizofanyika huko Anfield.

    Mane ambaye kwa sasa yuko nje ya dimba akiuguza jeraha la goti ameibuka kidedea akitangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa klabu na mchezaji bora wa mwaka chaguo la mashabiki akimshinda mshindi wa mwaka jana wa tuzo hiyo Mbrazil, Philippe Coutinho.

    Mane ameshinda tuzo hizo baada ya kuwa katika kiwango bora zaidi tangu alipotua Liverpool mwezi Agosti mwaka jana akitokea Southampton kwa ada ya Pauni Milioni 32.Mpaka sasa Mane ndiye mfungaji bora Liverpool akiwa amefunga mabao 13.

    Wengine waliochomoka na tuzo ni Trent Alexander-Arnold,18,aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi. Ben Woodburn ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Akademi.
               
    Emre Can ametwaa tuzo ya bao bora la mwaka baada ya bao lake la tiki taka alilofunga dhidi ya Watford wiki mbili zilizopita kuonekana kuwa bora zaidi kuliko mabao yote yaliyofungwa na Liverpool msimu wa wa 2016/17.

    Lucas Leiva amepewa tuzo ya heshima baada ya kufikisha miaka kumi (10) akiwa klabuni Liveroop.Tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa upande wa wanawake imeenda kwa Sophie Ingle.




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Sadio Mane mchezaji bora wa mwaka Liverpool,Can,Leiva wachomoka na tuzo Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top