Kampala,Uganda.
TIMU ya Kampala Capital City Authority maarufu kama KCCA jana Jumanne ilifanikiwa kutwaa kwa mara ya pili mfululizo ubingwa wa ligi kuu ya soka nchini Uganda maarufu kama Azam Uganda Premier League huku ikiwa imebakiza michezo miwili mkononi.
Mabao ya mikwaju ya penati ya Tom Masiko na Geofrey Sserunkuma katika dakika za 60 na 79 yaliipa KCCA ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya klabu ya Lweza kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Phillip Omondi huko Lugogo.
Ushindi huo umeifanya KCCA ifikishe pointi 60.Pointi 8 mbele ya SC Villa Jogoo wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na pointi 52 ambao hata kama watashinda michezo yao miwili iliyosalia hawataipiku KCCA ambayo sasa imetwaa ubingwa wa ligi kuu kwa mara ya 12.
Ikumbukwe KCCA ndiyo wawakilishi pekee wa Uganda kwenye michuano ya kimataifa
0 comments:
Post a Comment