Manchester, England.
MANCHESTER CITY imeendelea kujikusanyia matumaini ya kubaki katika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka nchini England baada ya mchana wa leo kuishushia Crystal Palace kichapo cha mbwa mwizi kwa kuifunga mabao 5-0 nyumbani Etihad Stadium.
David Silva ndiye aliyekuwa wa kwanza kuipa uongozi Manchester City baada ya kuifungia bao la kwanza katika dakika ya 2 tu mchezo.Bao hilo lilidumu mpaka mapumziko.
Bao la pili limefungwa na Nahodha Vincent Kompany katika dakika ya 49 huku bao la tatu likifungwa na Kevin De Bruyne katika dakika ya 59
Bao la nne limefungwa na Rahem Sterling katika dakika ya kwa mkwaju mkali wa karibu akiunganisha pasi ya kichwa iliyopigwa na mkongwe Pablo Zabaleta.
Nikolas Otamendi aliifungia Manchester City bao la tano katika dakika ya 90 kwa kichwa akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Kevin De Bruyne.Ushindi huo umeifanya Manchester City ikae nafasi ya tatu baada ya kufikisha pointi 69 kufuatia kushuka dimbani mara 35.
0 comments:
Post a Comment