WASHAMBULIAJI Amisi Tambwe na Obrey Chirwa wameirejesha Yanga SC kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara baada ya jioni ya leo kufunga mabao mawili ndani ya dakika tano na kuiwezesha miamba hiyo kuichapa Tanzania Prisons mabao 2-0 katika mchezo mkali wa ligi hiyo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.
Yanga SC ilipata bao lake la kwanza kupitia kwa Amisi Tambwe aliyefunga kwa kichwa katika dakika ya 70 akiunganisha krosi ya mlinzi wa kulia Juma Abdul Mnyamani aliyekuwa ameingia uwanjani muda mfupi uliopita kuchukua nafasi ya Hassan Kessy Ramadhani.
Dakika tano baadae yaani katika dakika ya 75 Obrey Chirwa aliifungia Yanga SC bao la pili kwa kichwa akiunganisha pasi ya kichwa kutoka kwa Amisi Tambwe aliyekuwa akiunganisha krosi safi kutoka wingi ya kushoto kwa Geoffrey Mwashiuya.
Ushindi huo umeifanya Yanga SC kufikisha pointi 59 na kuishusha Simba SC kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.Yanga SC ina michezo 26 wakati Simba SC ina michezo 27.
Katika mchezo mwingine Toto Africans imeifunga JKT Ruvu toka Pwani kwa mabao 2-1 katika mchezo mkali uliochezwa huko Mwanza kwenye dimba la CCM Kirumba.
Katika mchezo mwingine Toto Africans imeifunga JKT Ruvu toka Pwani kwa mabao 2-1 katika mchezo mkali uliochezwa huko Mwanza kwenye dimba la CCM Kirumba.
0 comments:
Post a Comment