728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 07, 2017

    Liverpool yabanwa nyumbani,Milner akosa penati baada ya miaka saba


    Liverpool,England.

    LIVERPOOL imeshindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani wa Anfield kujitengenezea mazingira mazuri ya kubaki kwenye kinyang'anyiro cha kusalia kwenye nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka nchini England baada ya leo jioni kulazimishwa sare ya bila kufungana na timu ngumu ya Southampton.

    Aidha katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Bobby Madley ilishuhudiwa nahodha wa Liverpool,James Milner akikosa penati kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka saba baada ya mkwaju wake wa penati kupanguliwa na kipa wa Southampton,Fraser
    Forster. 

    Mara ya mwisho kwa Milner kukosa mkwaju wa penati ilikuwa ni mwaka 2009 wakati huo alikuwa akiichezea Aston Villa na ilikuwa kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Bolton.Jumla Milner amefunga penati 19 katika maisha yake ya soka.

    Sare hiyo imeifanya Liverpool ibakie katika nafasi ya tatu ikiwa imefikisha pointi 70 baada ya kushuka dimbani mara 36.Manchester City inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 69 katika michezo 35.Manchester United nafasi ya tano ikiwa na pointi 65 baada ya kushuka dimbani mara 34.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Liverpool yabanwa nyumbani,Milner akosa penati baada ya miaka saba Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top