Paul Manjale, Dar Es Salaam.
KIUNGO wa Azam FC,Himid Mao Mkami ameondoka nchini usiku wa kuamkia leo kuelekea nchini Denmark kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Randers FC inayoshiriki ligi kuu ya nchi hiyo maarufu kama Danish Superliga.
Himid,24,atakuwa Randers kwa majaribio ya kipindi cha siku kumi (10) kisha baada ya hapo atarejea nchini na kuendelea na majukumu take ya kawaida klabuni kwake Azam FC.
Randers FC ilianzishwa Januari 1,2003 na hucheza michezo yake ya nyumbani kwenye uwanja wa AutoC Park Randers wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 11,000.
Mei 11,2006,Randers FC iliweka rekodi baada ya kuchukua ubingwa wa kombe la ligi ya Denmark (Danish Cup) kwa kuichapa Esbjerg bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Parken Stadium.Wakati huo Randers FC ilikuwa ligi daraja la kwanza.
0 comments:
Post a Comment