Libreville,Gabon.
TIMU ya taifa ya vijana ya Ghana ya chini ya umri wa miaka 17 maarufu kama Black Starlets imetabiriwa kutwaa ubingwa wa michuano ya AFCON ya vijana wa umri huo inayoendelea kutimua vumbi lake huko nchini Gabon.
Utabiri huo umetolewa na gwiji wa zamani wa Zambia, Kalusha Bwalya baada ya juzi Jumapili kukishuhudia kikosi hicho kikiianza michuano hiyo kwa mkwara mzito kwa kuishushia Cameroon kichapo kizito cha mabao 4-0 kwenye mchezo wa kundi A uliochezwa huko Stade Port-Gil.
Bwalya ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa kamati ya ufundi ya CAF amesema kwa namna Ghana waliovyotandaza soka safi na kuwapoteza vijana wenzao wa Cameroon hatashangaa kuona vijana hao wakitwaa ubingwa wa AFCON mwaka huu.
Mabao ya Ghana juzi Jumapili yalifungwa na Eric Ayiah pamoja na Ibrahim Sulley.Wote walifunga mabao mawili mawili.
Ghana itarejea tena uwanjani kesho Jumatano ya Mei 17 kwa kuvaana na wenyeji Gabon na iwapo itashinda mchezo huo itakuwa imefuzu nusu fainali na wakati huohuo itakuwa imekata tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la dunia itakayofanyika baadae mwaka huu nchini India.
0 comments:
Post a Comment