728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, May 08, 2017

    Diego Maradona arejea mzigoni


    Falme za kiarabu 

    GWIJI wa zamani wa soka wa Argentina,Diego Armando Maradona ametangazwa kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya Al-Fujairah Sports Club ya falme za kiarabu (UAE).

    Maradona mwenye umri wa miaka 56 sasa ameingia kandarasi ya mwaka mmoja kuinoa timu hiyo inayoshiriki ligi daraja la kwanza akipewa jukumu la kuipandisha timu hiyo mpaka ligi kuu maarufu kama Arabian Gulf League.

    Maradona amekuwa hana kazi tangu mwaka 2012 alipotupiwa virago na timu ya Al-Wasl ya Dubai ambako alihudumu kwa miezi 14 na siku 422 kabla ya kuonyeshwa mlango wa kutokea.

    Mara ya mwisho Fujairah kucheza ligi kuu ilikuwa ni msimu wa 2015/16 ambako walimaliza katika nafasi ya 13 na kushuka daraja baada ya kushinda michezo saba kati ya 26 wakionja kipigo katika michezo 14 na kushuka daraja kwa tofauti ya pointi moja.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Diego Maradona arejea mzigoni Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top