728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, May 08, 2017

    Real Madrid yasajili kinda la ajabu kwa pesa ya ajabu


    Rio de Janeiro,Brazil.

    REAL MADRID imeendelea kuonyesha kuwa huwa haina tabia ya kujivunga vunga pindi inapotaka kupata vitu vizuri na vya maana hii ni baada ya kuripotiwa kuwa imekubali kutoa dau la Euro Milioni 45 kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji kinda wa timu ya Flamengo  ya nchini Brazil, Vinícius José Paixão de Oliveira Júnior maarufu kama Vinicius Junior.

    Gazeti la Globoesporte ambalo linaaminika sana kwa habari za kimichezo nchini Brazil limesema Rais wa Real Madrid,Florentino Pérez ameweka dau hilo mezani na kuwapiku wapinzani wao Barcelona kwa tofauti ya Euro Milioni 20.


    Vinicius Junior mwenye umri wa miaka 16 sasa amevivutia vilabu vingi tajiri vya barani Ulaya vikiwemo Chelsea na Arsenal baada ya hivi karibuni kuibuka mchezaji bora na mfungaji bora wa michuano ya bara la Amerika Kusini ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ambapo Brazil iliibuka mabingwa. 

    Inadaiwa Vinicius Junior amechagua kujiunga na Real Madrid licha ya Barcelona kumtumia staa wake Neymar Jr kumshawishi kinda huyo ili akubali kuungana nae Camp Nou.

    Globoesporte limeendelea kufichua kwamba kila kitu kimekamilika kuhusu usajili wa Vinicius Junior kutua Real Madrid kinachosubiriwa sasa ni kinda huyo kufikisha miaka 18 hapo katikati ya mwaka 2018 baada ya fainali za kombe la dunia litakalofanyika nchini Urusi.

    Usajili wa Vinicius Junior utaigharimu Real Madrid jumla ya Euro Milioni 61 ikijumuisha mishahara pamoja na malipo ya wakala wake.Vinicius Junior atakuwa akilipwa mshahara wa Euro Milioni 8 kwa mwaka.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Real Madrid yasajili kinda la ajabu kwa pesa ya ajabu Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top