728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, May 17, 2017

    ANAONDOKA:Donald Ngoma anukia City


    Paul Manjale,Dar Es Salaam.

    HABARI KUBWA Jumatano ya leo kwenye mtandao maarufu wa michezo wa nchini Afrika Kusini wa KickOff.com ni kwamba mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga Mzimbabwe, Donald Ndombo Ngoma yuko mbioni kumwaga wino wa kuichezea klabu ya Polokwane City ya nchini humo.

    Chanzo cha karibu kabisa na klabu hiyo,kimesema Polokwane City inatarajia kukamilisha usajili huo hivi karibuni.

    "Mazungumzo yamefikia katika hatua nzuri.Ngoma anaweza akamwaga wino muda wowote kuanzia sasa".Kimesema chanzo hicho.

    Ngoma alijiunga na Yanga mwaka 2015 akitokea FC Platinums ya nyumbani kwao Zimbabwe na kutengeneza safu kali ya ushambuliaji na Mrundi,Amisi Tambwe ambayo imefanikiwa kuipa Yanga makombe mawili ya ligi kuu bara pamoja na kombe moja la michuano ya FA.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ANAONDOKA:Donald Ngoma anukia City Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top