728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 14, 2017

    Aliyewahi kukipiga Mamelodi Sundowns na SuperSport atua Singida United


    Paul Manjale,Dar Es Salaam.

    KAMA mambo yatakwenda kama yalivyopangwa wageni wa ligi kuu bara,Singida United watatangaza kukamilisha usajili wa Mshambuliaji wa Kimataifa wa Zimbabwe,Simbarashe "Simba" Nhivi Sithole maarufu kama Simba Nhivi.

    Nhivi mwenye umri wa miaka 26 aliwasili jijini Dar Es Salaam jana Jumamosi akitokea nchini kwao Zimbabwe na kupokelewa na kocha wa Singida United, Mholanzi Hans van der Pluijm tayari kuweka mambo kadhaa sawa kabla ya kusaini mkataba wa kujiunga na timu hiyo inayomilikiwa na Mfanyabiashara Maarufu nchini Yusuph Mwandami.

    Ikiwa usajili huo utakamilika Nhivi atakuwa ni mchezaji wa nne kukiunga na Singida United katika kipindi kisichozidi miezi miwili.Wengine ni Elisha Muroiwa,Wisdom Mutasa na Raphael Kutinyu.


    Msimu uliopita Nhivi alishika nafasi ya pili kwenye orodha ya wafungaji bora wa CAPS United akifunga mabao saba. Mabao manne nyuma ya Mkongwe,Leonard Tsipa aliyetwaa kiatu cha dhahabu baada ya kufunga mabao 11 na kuiwezesha CAPS United kutwaa ubingwa wake wa kwanza wa ligi kuu ya Zimbabwe tangu mwaka 2005.

    Nhivi pia alikuwa sehemu ya kikosi cha CAPS United ambacho msimu huu kilifuzu hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa Afrika baada ya kuwatoa mabingwa mara tano wa michuano hiyo,TP Mazembe ya Congo DRC.Hivi karibuni Nhivi alijiuengua kuichezea CAPS United baada ya kushindwa kufiakia makubaliano ya kuongeza mkata mpya.

    Kabla ya kutua CAPS United, Nhivi aliwahi kuzichezea timu za Shooting Stars na Dynamos za nyumbani kwao Zimbabwe pamoja na timu za Afrika Kusini za Mamelodi Sundowns na SuperSport.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Aliyewahi kukipiga Mamelodi Sundowns na SuperSport atua Singida United Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top