728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 14, 2017

    Man City yaanza kupangua kikosi chake,Yampa mkono wa kwaheri mlinzi Pablo Zabaleta

    Manchester, England.
    MANCHESTER CITY imeanza kuondoa wachezaji isiyowahijitaji kwenye kikosi chake cha msimu ujao hii ni baada ya kutangaza kuwa itaachana na mlinzi wake wa siku nyingi Muargentina,Pablo Zabaleta hapo mwishoni mwa msimu huu.
    Taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Manchester City imesema Zabaleta ataondoka siku chache zijazo na kuhitimisha miaka yake tisa ya utumishi uliotukuka klabuni hapo na kwenda kujiunga Westham United kwa mkataba wa miaka miwili.
    Jana Jumamosi Zabaleta alipewa heshima ya kupigiwa makofi na mashabiki baada ya kuingia uwanjani dakika za mwisho mwisho kwenye mchezo ambao Manchester City iliweka juu matumaini yake ya kumaliza kwenye nafasi nne za juu baada ya kuifumua Leceister City mabao 2-1.Manchester City captain Vincent Kompany tweeted a farewell message to Zabaleta
    Zabaleta alijiunga na Manchester City mwaka 2008 kwa ada ya £6.5m akitokea Espanyol ya Hispania.Siku moja kabla ya Bilionea Sheikh Mansour wa Abou Dhabi kutangazwa kuwa mmiliki mpya wa klabu hiyo.
    Zabaleta anaiacha Manchester City akiwa na kumbukumbu nzuri ya kuichezea jumla ya michezo 332.Akitwaa kombe la ligi kuu mara mbili,kombe la FA,kombe la ligi (Capital One) na Ngao ya jamii.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Man City yaanza kupangua kikosi chake,Yampa mkono wa kwaheri mlinzi Pablo Zabaleta Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top