728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, May 14, 2017

    Mo ajiondoa Simba SC kisa SportPesa , Aidai Simba 1.4 billion



    Faridi Miraji , Dar es salaam.                      

    Mwanachama wa Simba Mohamed Dewji maarufu kama MO amewandikia 'demand note' viongozi wa Simba Kwa kukiuka makubaliano waliyokubaliana ya mpango kuwekeza Simba, Timu ya Simba walikubaliana kubadili Mfumo wa uendeshaji wa klabu. wanachama wakafanya mabadiliko ya katiba ili MO aweze kuwekeza Nia ya Mohamed Dewji 'Mo ' ni kuwekeza hisa asilimia 51 zenye dhamani  Bilioni 20 lakini mpango huo utakufa muda wowote Baada ya Simba kukiuka makubaliano.

    Mohamed Dewji ameamua kusitisha mpango huo kutokana na viongozi wa Simba kuingia mkataba na kampuni ya SportPesa bila kumshirikisha.  Mohamed Mo anataka kulipwa Pesa zake zote alizokuwa anazitoa Tangu mwaka Jana kulipa mishahara ya wachezaji na bechi la ufundi la Simba. MO ambaye aliipa Simba Msaada wa Milioni 100 kwenda kwenye dirisha la usajili mwaka Jana na pia alikuwa na mpango wa kuikopesha Simba bilioni Moja ambaye wangeiweka kwenye mpango wa uwekezaji. 

    Mohamed Dewji 'Mo ' amewaandika viongozi wa Simba Demand Note Kwa kukiuka makubaliano yao Kwani walikubaliana na uongozi atoe Pesa kama makubaliano ya kuingia kwenye hisa ila Ikitokea kampuni inataka kuidhamini ilitakiwa viongozi wa Simba na MO wakae meza moja ili kampuni inayoidhamini Simba itambue Mwelekeo wa Simba. ili Isije ikaleta mkanganyiko huko Mbele 

    Kutokana na makubaliano hayò viongozi wa Simba wameingia mkataba na SportsPesa kimyakimnya bila Mohamed Dewji Mo kushirikishwa. Jana Simba wametambulisha kampuni ya SportPesa kuwa wadhamini kinyume na makubaliano yao na Mo.  

    Simba wameingia mkataba wa miaka mitano na kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa ambao una thamani ya Sh bilioni 4.9. Mkataba huo, utaifanya Simba ipokee kitita cha Sh milioni 888 katika mwaka wa kwanza. Na watapewa Bilioni moja na Milioni 80 mwaka wa mwisho wa mkataba. Pia fedha hizo zitakuwa Zinaongezeka %5 kila mwaka 

    Kama hivyo haitoshi, Simba imepewa motisha iwapo watachukua ubingwa wa ligi kuu watapewa milioni 100 Huku Sportpesa wakitenga Sh milioni 250 iwapo Simba wakibeba Kombe la Kagame au michuano iliyo chini ya Caf.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Mo ajiondoa Simba SC kisa SportPesa , Aidai Simba 1.4 billion Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top