728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, April 02, 2017

    WAMEKAA:Simba SC yagomewa na Kagera Sugar,yafa 2-1 Kaitaba


    Kagera,Tanzania.

    Simba SC imeshindwa kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya jioni ya leo kufungwa mabao 2-1 na Kagera Sugar katika mchezo mkali uliochezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

    Wenyeji Kagera Sugar ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao baada ya mshambuliaji wake hatari Mbaraka Yusuph kufunga kwa shuti kali la mbali katika dakika ya 27 ya kipindi cha kwanza.Bao hilo lilidumu mpaka mapumziko.

    Edward Christopher aliifungia Kagera Sugar bao la pili dakika ya 46 kwa shuti la karibu akiunganisha vyema krosi safi kutoka wingi ya kulia na kumwacha kipa wa Simba SC,Mghana Daniel Ageyi akiwa hana la kufanya.bao la Simba SC limefungwa na Muzamiru Yasin katika dakika ya 61.

    Nyota katika mchezo wa leo aliikuwa ni kipa wa Kagera Sugar,Juma Kaseja aliyeinyima Simba SC baada ya kuokoa michomo mingi ya hatari iliyokuwa ikielekezwa langoni kwake.

    Kichapo hicho kimeibakisha Simba SC katika nafasi ya pili na alama zake 55,alama moja nyuma ya yanga yenye alama 56.Timu zote zimecheza michezo 25.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WAMEKAA:Simba SC yagomewa na Kagera Sugar,yafa 2-1 Kaitaba Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top