Paul Manjale
TIMU ya AFC Eskilstuna ya Mtanzania,Thomas Ulimwengu imeuanza vibaya msimu wake wa kwanza kwenye ligi kuu ya soka nchini Sweden ( Allsvenskan) baada ya Jumapili Usiku kufungwa mabao 3-1 na GIF Sundsvall katika mchezo mkali wa ligi hiyo uliochezwa ugenini kwenye uwanja wa Norrporten Arena na kushuhudiwa na watazamaji 3,549.
Wageni AFC Eskilstuna ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika dakika ya 25 ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji wake Mserbia,Sasa Matic.
Kuingia kwa bao hilo kuliwaamsha wenyeji GIF Sundsvall ambao walikuja juu na kufanikiwa kusawazisha bao hilo katika dakika ya 31 kupitia kwa Peter Wilson kabla ya kuongeza mengine mawili katika dakika za 41 na 52 kupitia kwa Lars Christian Krogh Gerson na Marcus Danielsson.
Aidha katika mchezo huo ambao Ulimwengu hakuwemo kikosini kutokana na kuwa majeruhi ilishuhudiwa kiungo wa zamani wa Arsenal,Mghana Emmanuel Frimpong akicheza kwa dakika zote tisini na kuambulia kadi moja ya njano.
Kichapo hicho kimeipeleka AFC Eskilstuna mkiani kabisa mwa ligi hiyo yenye timu 16 huku GIF Sundsvall ikikaa kileleni baada ya kujikusanyia alama tatu katika mchezo mmoja.
Vikosi
Gif Sundsvall (3-5-2): Tommy Naurin -Marcus Danielsson, Eric Björkander, Noah Sonko Sundberg - Eric Larsson, Lars Christian Krogh Gerson, Smajl Suljevic,Kristinn Steindorsson (Romain Gall 83),Dennis Olsson - Kristinn Freyr Sigurdsson (Jonathan Morsay (73), Peter Wilson (Linus Hallenius 72).
AFC Eskilstuna (4-4-2) : Tim Erlandsson -Daniel Björnkvist, Ludvig Öhman Silwerfeldt, Alexander Michel, Jernade Meade - Thomas Piermayr,Emmanuel Frimpong, Anel Rashkaj, Omar Eddahri (Ferid Ali 57) - Mohamed Buya Turay,Sasa Matic (Mauricio Albornoz 70).
0 comments:
Post a Comment