Granada,Hispania.
IKICHEZA bila ya staa wake mkubwa,Lionel Messi Barcelona aliyefungiwa Barcelona imeibuka na ushindi mnono ugenini baada ya Jumapili Usiku kuwafunga wenyeji wao Granada mabao 4-1 huko Estadio Nuevo Los Carmenes.
Barcelona imejipatia mabao yake kupitia kwa Luis Suarez,Paco Alcacer,Ivan Rakitic na Neymar aliyekuwa akifikisha bao lake la 100 tangu ajiunge na miamba hiyo mwaka 2013 akitokea Santos.Bao la Granada limefungwa na Jeremie Boga huku beki wake Uche Agbo akitolewa uwanjana kwa mchezo mbaya.
Ushindi huo umeifanya Barcelona iendelee kushika nafasi ya pili baada ya kufikisha alama 66.Alama mbili nyuma ya vinara Real Madrid wenye alama 68 wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Katika mchezo wa mapema Real Madrid ikiwa nyumbani Santiago Bernabeu iliifunga Alaves mabao 3-0 kwa mabao ya Karim Benzema Isco na Nacho.
0 comments:
Post a Comment