Dar Es Salaam,Tanzania.
AFRICAN LYON imejinasua kutoka kwenye mstari mwekundu wa kushuka daraja baada ya mchana wa leo kuifunga Stand United ya mkoani Shinyanga kwa bao 1-0 katika mchezo mkali wa ligi kuu bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.
Bao pekee la mchezo huo uliochezwa majira ya saa 8:00 mchana na kushuhudiwa na watazamaji wachache sana limefungwa katika kipindi cha kwanza na Abdalah Mguhi.
Ushindi huo umeipeleka African Lyon mpaka nafasi ya 10 kwa muda kwenye msimamo wa ligi kuu bara baada ya kufikisha alama 29 katika michezo 25.Stand United iko nafasi ya11 ikiwa na alama zake 28.
0 comments:
Post a Comment