London,England.
Wakati dunia ya soka ikiamini kuwa Arsenal inahitaji mshambuliaji mpya wa kiwango cha juu ili iweze kuwa mshindani wa kweli katika michuano ya ligi kuu pamoja na ligi ya mabingwa kocha wa klabu hiyo Arsene Wenger yeye ameendelea kupinga suala hilo na kusisitiza haitaji mshambuliaji mpya.
Mapema wiki iliyopita gwiji wa zamani wa klabu hiyo Thierry Henry ambaye kwasasa ni mchambuzi wa soka aliishauri klabu hiyo kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Karim Benzema ili kuongeza nguvu kikosini.Henry alisema Arsenal ikimsajili Benzema itakuwa mshindani wa kweli na inaweza kutwaa ubingwa wa ligi kuu akisifia uwezo wa nyota huyo katika kufumania nyavu na kusisitiza kuwa Olivier Giroud peke yake hana uwezo wa kuipa Arsenal mataji makubwa.
Lakini kama ilivyoada kocha Arsene Wenger ameendelea kupinga karibu kila ushauri anaopewa kuhusu kuboresha kikosi chake.Akiongea jana jumamosi Wenger anaamini atafanya vizuri kwa kuwatumia nyota waliopo kama Giroud, Theo Walcott, Alexis Sanchez, Mesut Ozil na Alex-Oxlade Chamberlain kuliko kuwa na mshambuliaji Karim Benzema.
Wenger amesema
"Nauheshimu sana ufahamu wa Thierry Henry katika masuala ya soka lakini jambo hilo halipo kimahesabu kama anavyodhani,"
"Tunapaswa kuendelea na uchezaji wetu wa pamoja kuliko kumtegemea mtu mmoja aje atufungie magoli.
"Nafikiri Olivier Giroud asingeshindwa kufunga magoli 20 msimu uliopita kama angecheza mechi zote vivyo hivyo pia kwa Theo Walcott.
"Sioni sababu mtu kama Alex Oxlade Chamberlain asiwe na kiu ya kufunga japo goli 10 kwa msimu, Sanchez anafunga pia.Ozil anapaswa kuafunga goli 10.Kwa mtu anayecheza nyuma ya mshambuliaji mkuu anapaswa kufunga goli za kutosha.Kikubwa ni kugawana kila mmoja afunge kadri awezavyo.
0 comments:
Post a Comment