London,England.
Klabu ya Chelsea imeanza vibaya kuutetea ubingwa wake wa ligi kuu ya England baada ya kulazimishwa sare ya goli 2-2 na klabu ya Swansea City katika mchezo mkali uliopigwa jioni ya leo katika dimba la Stamford Blidge.
Chelsea ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa kiungo wake Oscar (23') kisha Swansea wakasawazisha dakika ya (29) kupitia kwa nyota wake mpya Andre Ayew.Dakika moja baadae yaani dakika ya 30 Chelsea ilipata goli la pili baada ya mlinzi wa Swansea Federico Fernández kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa shuti la Willian.
Dakika ya 55 Swansea ilisawazisha goli hilo kwa mkwaju wa penati uliofungwa kwa ustadi mkubwa na mshambuliaji Mfaransa Batefimbi Gomis.Swansea walipata mkwaju huo baada ya Gomis kuangushwa katika eneo la hatari na mlinda mlango wa Chelsea Thibaut Courtois ambaye alilimwa kadi nyekundu kufuatia tukio hilo.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho......
Arsenal v Westham
Newcastle v Southampton
Stoke v Liverpool
0 comments:
Post a Comment