Paul Manjale,Dar Es Salaam.
YANGA imeishusha kwa muda Simba kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL) baada ya jioni ya leo kuichapa Azam FC kwa bao 1-0 katika mchezo mkali wa ligi hiyo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.
Bao pekee la mchezo huo limefungwa katika dakika ya 71 na mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia,Obrey Chirwa kwa shuti kali baada ya kuunasa mpira mrefu uliopigwa na kiungo,Haruna Niyonzima na kuwazidi maarifa mabeki wawili wa Azam FC na kumfunga kirahisi mlinda mlango,Aishi Manula.
Huo umekuwa ni ushindi wa kwanza kwa Yanga dhidi ya Azam kwenye ligi kuu bara tangu Machi 2013.
Aidha katika mchezo huo timu hizo zililazimika kufanya mabadiliko la lazima baada ya kuwapoteza nyota wao wawili kwa majeruhi katika kipindi cha kwanza.Yanga ilimpoteza Justine Zulu huku Azam ikimpoteza Yahya Mohamed.
0 comments:
Post a Comment