728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, February 10, 2017

    Arsenal yanasa kinda la miaka 13 linalofananishwa na Memphis Depay

    London,England.

    ARSENAL imefanikiwa kumnasa kinda wa Nigeria aliyezaliwa Marekani,Lateef Omidiji Jr.

    Arsenal imemnasa Omidiji Jr mwenye umri wa miaka 13 baada ya kushinda vita dhidi ya vilabu vya Chelsea,Liverpool,Barcelona na Real Madrid ambazo navyo vilionyesha nia ya kuhitaji huduma ya kinda huyo anayefananishwa kiuchezaji na winga wa zamani wa Man United,Memphis Depay.

    Habari zaidi zinasema Omidiji Jr atakuwa akisafiri kila mwisho wa msimu kwenda London kufanya mazoezi klabuni Arsenal mpaka hata atakapokuwa amefikia umri wa kusaini mkataba wa kulipwa.

    Omidiji Jr ni zao la kikosi cha vijana cha Sparta Rotterdam ya Uholanzi ambacho kimewahi kuwa na nyota kama Memphis Depay na Georginio Wijnaldum.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Arsenal yanasa kinda la miaka 13 linalofananishwa na Memphis Depay Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top