Sagamu,Nigeria.
KOCHA wa Nigeria,Gernot Rohr,ameunga mkono hatua ya nyota wake John Mikel Obi na Odion Ighalo ambao mwezi uliopita waliamua kuihama ligi kuu nchini England na kwenda kucheza soka nchini China na kujiunga na vilabu vya Tianjin Teda na Changchun Yatai.
Rohr mzaliwa wa Ujerumani amesisitiza kuwa uwamuzi huo ni mzuri kwa maendeleo ya wachezaji hao na taifa zima la Nigeria.Aidha Rohr ametupilia mbali hofu kwamba uhamisho huo utashusha viwango vya wachezaji hao kwa madai kuwa ligi ya China haina changamoto kubwa.
Rohr amesema ligi ya sasa ya China ni tofauti sana na ile ya zamani kwani sasa China ina ligi bora sana na kandanda lake ni hali ya juu na imekusanya wachezaji bora kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Ameongeza kwenda China kucheza soka mara kwa mara ni bora mara mia kuliko kukaa benchi katika vilabu vya Chelsea na Watford.
"Jambo la kwanza kufahamu ni kwamba,hawa wachezaji walikuwa hawachezi kabisa kwenye vilabu vyao vya zamani Mikel (Chelsea) na Ighalo (Watford).Kwa kuwa sasa wamehamia kwenye vilabu vipya hii ina maana kwamba watakuwa wakicheza mara kwa mara.
"Hii ni nzuri kwa Nigeria,nzuri pia kwa kiu yetu ya kuwepo kwenye fainali za kombe la dunia la mwaka 2018 nchini Urusi.
0 comments:
Post a Comment