Abu Dhabi,Falme za Kiarabu.
Zamalek vidume mwanangu.Usiku wa kuamkia leo Jumamosi wametwaa ubingwwa wao wa tatu wa Super Cup ya Misri baada ya kuwachapa mahasimu wao wakubwa Al Ahly kwa penati 3-1 kufuatia sare ya bila kufungana katika muda wa kawaida.
Katika mchezo huo uliochezwa katika dimba la Sheikh Mohammed Bin Zayed huko Abu Dhabi ,Falme za Kiarabu ilishuhudiwa kipa wa Zamalek,Mahmoud Genesh akiibuka shujaa baada ya kupangua penati mbili za Al Ahly za Momen Zakaria na Saleh Gomaa.
Vikosi
Al Ahly XI: Sherif Ekramy; Mohamed Hany,Saad Samir, Ahmed Hegazy, Hussein El-Sayed; Hossam Ashour, Ahmed Fathi; Walid Soliman, Abdallah El-Said, Momen Zakaria;Junior Ajayi.
Zamalek XI: Mahmoud Genesh; Osama Ibrahim, El-Wensh, Ali Gabr, Mohamed
Nassef; Moruf Youssef, Tarek Hamed,Ahmed Tawfik; Mohamed Ibrahim, Stanley Ohawuchi, Bassem Morsy.
0 comments:
Post a Comment