St.Truiden,Ubelgiji.
NAHODHA wa Tanzania,Mbwana Ally Samatta (pichani) akipongezwa na mchezaji mwenzake baada ya kuifungia Genk bao moja dakika ya 39 katika ushindi wa mabao 3-0 jana usiku dhidi ya St.Truiden huko Staaien.
Mabao mengine ya Genk yamefungwa na Alejandro Pozuelo Melero aliyefunga bao la kwanza dakika ya 37' huku bao la tatu likifungwa na Ruslan Malinovskiy dakika ya 45'.
Ushindi huo umeipeleka Genk nafasi ya 5 kwa muda baada ya kufikisha pointi 41 katika michezo 26 na kuishusha Gent yenye pointi 40 katika michezo 25.
St.Truiden imesalia katika nafasi ya 11 na pointi zake 26 katika michezo 26.
0 comments:
Post a Comment