728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, August 14, 2016

    UCHAMBUZI. BOURNEMOUTH VS MANCHESTER UNITED

    Na.Chikoti Cico.



    The Vitality Stadium (SAA 9:30 ALASIRI) Katika kufungua pazia la ligi kuu nchini Uingereza klabu ya Bournemouth itaikaribisha Manchester United kwenye wao wa Vitality Stadium mchezo unaotarajiwa kuwa wa vuta nikuvute katika kutafuta alama tatu za mapema. 

     TAARIFA ZA TIMU: 

     Bournemouth Kuelekea mchezo huo kocha wa Bournemouth Eddie Howe atamkosa winga wake Junior Stanislaus ambaye anasumbuliwa na matatizo ya ngiri. MANCHESTER UNITED Klabu ya Manchester United itacheza mchezo huo bila ya Paul Pogba na Chris Smalling ambao wamesimamishwa kwa nyakati tofauti, Pogba alionyeshwa kadi ya pili ya njano kwenye mchezo wa fainali ya Coppa Italia akiwa bado anaichezea klabu ya Juventus ikifuatia kadi ya kwanza aliyoonyeshwa kwenye mchezo wa nusu fainali na hivyo kusimamishwa kwa mchezo mmoja, adhabu ambayo ataitumikia kwenye mchezo huo dhidi ya Bournemouth. Naye baki wa katikati wa United Chriss Smalling alisimamishwa baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa fainali ya kombe la FA Cup dhdi ya Crystal Palace.
     

    TAKWIMU KUELEKEA MCHEZO HUO: 

    Klabu ya Bournemouth haijafungwa kwenye michezo minne iliyopita waliyocheza nyumbani dhidi ya Manchester United katika mashindano mbalimbali, wameshinda michezo miwili na kutoka sare michezo miwili. Michezo minne kati ya mitano ambayo Manchester United ilifungwa katika kufungua pazia la ligi ya primia, United walifungwa ugenini. Nahodha wa United Wayne Rooney amefunga magoli mengi kwenye michezo ya kufungua pazia la ligi iliyochezwa wikendi kuliko mchezaji mwingine yeyote anayecheza kwasasa ndani ya ligi ya primia, amefunga magoli sita. Kocha wa United Jose Mourinho ameshinda michezo sita na kutoka sare mchezo mmoja katika michezo saba iliyopita aliyocheza kufungua pazia la ligi ya primia. Takwimu pia zinaonyesha klabu hizi mbili zimekutana mara 10 kwenye ligi ya primia na Bournemouth imeshinda mara mbili na Manchester United imeshinda mara sita na wametoka sare mara mbili.

    VIKOSI VINAWEZA KUWA HIVI: 

    Bournemouth XI: Federici; Francis, Aké, Cook, Daniels; Ibe, Surman, Arter, Pugh; Wilson, King Manchester United XI: De Gea; Valencia, Bailly, Blind, Shaw; Carrick, Fellaini; Mkhitaryan, Rooney, Martial; Ibrahimović
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: UCHAMBUZI. BOURNEMOUTH VS MANCHESTER UNITED Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top