Corinthians, Brazil.
BRAZIL U23 imefanikiwa kufuzu nusu fainali ya michuano ya Olimpiki kwa upande wa soka la wanaume baada ya leo alfajiri kuifunga Colombia U23 kwa jumla ya mabao 2-0 katika mchezo wa robo fainali uliochezwa katika uwanja wa Arena Corinthians.
Brazil imepata mabao yake kupitia kwa nahodha wake,Neymar 14' aliyefunga kwa mkwaju wa faulo pamoja na Luan 85'
Brazil sasa itacheza na Honduras katika mchezo wa nusu fainali utakaochezwa siku ya Jumatano.Honduras imefika hatua hiyo baada ya kuichapa Korea Kusini kwa bao 1-0 lililofungwa na A Elis dakika ya 58 huko Estadio Mineirao.
Vikosi
Colombia: Bonilla, Tesillo, D.Balanta,Lerma, Pabon,Gutierrez (C), Preciado,Roa, Palacios, Barrios, C.Borja
Brasil: Weverton, Zeca, R.Caio,Marquinhos, R.Augusto, D.Santos, Luan,G.Barbosa, Neymar (C), G.Jesus,Walace
Timu zilizotinga nusu fainali ni Ujerumani,Brazil,Nigeria na Honduras
Ratiba ya Nusu fainali Jumatano
Ujerumani v Nigeria
Brazil v Honduras
0 comments:
Post a Comment