728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, August 14, 2016

    UCHAMBUZI: ARSENAL VS LIVERPOOL -EMIRATES (SAA 12 JIONI)

    Chikoti Cico



    Pazia la ligi kuu nchini Uingereza limefunguliwa Jumamosi ya tarehe 13 mwezi Agasti kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali, Jumapili pazia la ligi hiyo litafunguliwa kwa mchezo jati ya Arsenal vs Liverpool. 

    TAARIFA ZA TIMU: ARSENAL

    Klabu ya Arsenal kuelekea mchezo huo imekuwa na matatizo kwenye eneo la ulinzi, mabeki wake wawili Per Mertesacker na Gabriel wote ni majeruhi huku Laurent Koscielny akitegemewa kucheza ingawa hakuchezo mchezo wowote wa maandalizi ya ligi (pre season). Pia Klabu hiyo chini ya kocha Arsenal Wenger itawakosa Danny Welbeck na Carl Jenkison ambao ni majeruhi huku mshambuliaji Olivier Giroud akiwa na hatihati ya kutokucheza mchezo huo dhidi ya Liverpool kutokana na kuwa majeruhi. LIVERPOOL. Liverpool wanaweza kufungua pazia la ligi ya primia bila ya wachezaji wao Daniel Sturridge na James Milner ambao wote ni majeruhi na hivyo kukiwa na hatihati ya kucheza dhidi ya Arsenal, Kipa Loris Karius na beki Mamadou Sakho ambao pia ni majeruhi hawatacheza mchezo. Kuelekea mchezo huo wachezaji Dejan Lovren na Marko Grujic ambao walikuwa na maumivu ya michezo ya “pre season” wako fiti kwasasa kupambana dhidi ya washika bunduki wa jiji la London.

    TAKWIMU MBALIMBALI KUELEKEA MCHEZO HUO

    Klabu ya Arsenal imepoteza mchezo mmoja tu kati ya michezo tisa iliyopita ya ligi ya primia waliyokutana na Liverpool, huku wakishinda michezo minne na kutoka sare michezo minne. Pia Arsenal wamepoteza michezo miwili tu kati ya michezo 15 iliyopita ya nyumbani kwenye kufungua pazia la ligi ya primia huku wakishinda michezo 10 na kutoka sare michezo mitatu pekee yake. Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Girioud amefunga magoli manne katika michezo minne iliyopita aliyocheza dhidi ya Liverpool kwenye ligi ya primia, Katika mwaka 2016 Liverpool inaongoza kwa kufunga magoli mengi kwenye ligi ya primia kuliko timu nyingine yoyote ile, mpaka sasa wamefunga magoli 41. Kiungo wa Liverpool Roberto Firmino amehusika kwenye magoli 13 (magoli tisa na “assist” nne) ya klabu hiyo katika michezo 15 ya ligi ya primia aliyocheza kwa mwaka 2016, magoli hayo yanahusisha magoli mawili aliyowafunga klabu ya Arsenal hapo mwezi Januari kwenye msimu uliopita wa ligi. Mchezo kati ya Arsenal vs Liverpool umehusisha magoli mengi ya “hat trick” kuliko mchezo wowote mwingine kwenye ligi ya primia, mpaka sasa ni “hat trick”tano zimeshafungwa. Takwimu za ligi pia zinaonyesha kwamba klabu hizi mbili zimekutana mara 220 na Arsenal imeshinda mara 78 huku Liverpool ikishinda mara 83 na wametoka sare mara 59. 
     

    VIKOSI VINAWEZA KUWA HIVI:

    Arsenal XI: Cech; Bellerin, Holding, Monreal, Gibbs; Xhaka, Cazorla; Chamberlain, Ramsey, Walcott; Sanchez

    Liverpool XI: Mignolet; Clyne, Lovren, Klavan, Moreno; Emre Can, Henderson; Mane, Lallana, Coutinho; Firmino
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: UCHAMBUZI: ARSENAL VS LIVERPOOL -EMIRATES (SAA 12 JIONI) Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top