Munich,Ujerumani.
MPANGO wa klabu ya Real Madrid wa kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Bayern Munich,David Alaba,umegonga mwamba baada ya klabu hiyo ya Ujerumani kuikataa ofa yake ya €65m.
Habari za kuaminika kutoka Ujerumani zinasema,Rais wa klabu ya Bayern Munich,Karl-Heinz Rummenigge tayari amefanya mawasiliano na wawakilishi wa Alaba na kuwataarifu kuwa ofa ya €65m iliyotoka Madrid imekataliwa na klabu yake na nyota huyo anayetumia vyema mguu wa kushoto ataendelea kubaki na miamba hiyo ya Allianz Arena.
Wakati huohuo taarifa kutoka AS zinasema Bayern Munich itakuwa tayari kuketi tena katika meza ya mazungumzo ikiwa tu Real Madrid itakuja na ofa inayofikia angalau €80m.
Hii ni mara ya pili ndani ya kipindi kifupi kwa Bayern Munich kukataa ofa iliyotoka Real Madrid kwa ajili ya Alaba.Mara ya kwanza ni mwezi Juni pale ilipokataa ofa ya €50m.
0 comments:
Post a Comment