Bournemouth,England.
JOSE Mourinho amekianza vyema kibarua chake cha kuinoa Manchester United baada ya mchana huu kukiongoza kikosi chake kuichapa AFC Bournemouth kwa mabao 3-1 katika mchezo mkali wa ligi kuu England uliochezwa katika uwanja wa Vitality Stadium.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na Mwamuzi,Andre Marriner,Manchester United imejipatia mabao hayo kupitia kwa Juan Mata 40',Wayne Rooney 58 na Zlatan Ibrahimovic 64' bao la AFC Bournemouth limefungwa na Mlinzi,Adam Smith 69'
Matokeo hayo yameifanya Manchester United kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu England kwani hakuna timu yoyote ambayo mpaka sasa imefunga mabao matatu.
Takwimu
Umiliki (Possesion):Manchester United imemiliki mchezo kwa asilimia 53,Bournemouth 47.
Mchezaji Bora wa Mechi:Wayne Rooney
Vikosi.
Bournemouth XI: Boruc,Francis, Adam Smith, Steve Cook,Daniels, Ibe, Surman, Arter, Lewis Cook,Wilson, King
Manchester United XI: De Gea,Valencia, Bailly, Blind, Shaw, Fellaini,Herrera, Mata, Rooney, Martial,Ibrahimovic
0 comments:
Post a Comment