728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, July 01, 2016

    NOLITO ATUA MAN CITY NA KUPEWA JEZI NAMBA 9

    Manchester, England.

    Manchester City imeendelea kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya England na michuano minne baada ya leo hii kumsajili Manuel Arago maarufu kama Nolito toka Celta Vigo kwa ada ya £13.8m.

    Nolito,29,amesaini mkataba wa miaka minne wa kuitumikia miamba hiyo ya jiji la Manchester City na atakuwa akivaa jezi namba tisa kwa kipindi chote atakachohudumu Etihad.

    Nolito anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Manchester City tangu miamba hiyo ilipoanza kuwa mikononi mwa kocha Pep Guardiola.Wengine ni Ilkay Gundogan na Aaron Moy.

    Akiwa na Celta Vigo,Nolito alifanikiwa kufunga mabao 39 katika michezo 100 ya La Liga.Vilabu vingine alivyowahi kuvichezea Nolito ni Benfica pamoja na Granada.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NOLITO ATUA MAN CITY NA KUPEWA JEZI NAMBA 9 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top