728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, July 01, 2016

    PICHA LINAENDELEA!!TFF YAZUIA MAMILIONI YA YANGA SC

    Dar es Salaam,Tanzania.

    YANGA walitakiwa kupewa Sh milioni 50 ikiwa ni zawadi ya kuchukua Kombe la Shirikisho (FA), baada ya kuifunga Azam
    mabao 3-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa Mei 25 mwaka huu kwenye
    Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

    Kutokana na Yanga kudaiwa ushuru wa vifaa vya michezo vilivyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa ajili ya michuano ya makundi ya Kombe la Shirikisho sasa fedha hizo zimezuiliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

    Rais wa TFF, Jamal Malinzi, amesema jana kuwa Yanga walishindwa kulipia ushuru vifaa hivyo vilivyotakiwa kutumika katika mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), uliochezwa Jumanne wiki hii,kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

    Malinzi alisema TFF ilitumia fedha zake kuwalipia Yanga ushuru wa vifaa hivyo  na hawatatoa fedha za zawadi za kombe FA mpaka pale watakapolipa deni wanalodaiwa na shirikisho hilo.

    Kauli ya Malinzi imekuja baada yaviongozi wa Yanga kushindwa kuitikia wito wa TFF wa kwenda kupiga hesabu ya madeni wanayodaiwa.

    “Fedha za zawadi za Kombe la FA tumepewa na Azam ambao ndio walikuwa wadhamini ila
    tumewaambia ndugu zetu njooni tupige hesabu  mpaka sasa hawajafika,” alisema Malinzi.

    Malinzi alisema awali alimwagiza katibu mkuu wa TFF, Celestin Mwesigwa, kukaa na viongozi wa Yanga ili kujua madeni wanayodaiwa, lakini hawakuitikia wito huo.

    “Niwape tu mfano, vifaa vya Yanga vimekuja kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Shirikisho, lakini hawajatoa hata shilingi 10 za kulipia ushuru, tukija kwa yule nyota wao wa kimataifa, Obrey Chirwa, tulitoa fedha katika upatikanaji wa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) yake hivyo wanapaswa kuja
    tukae mezani,” alisema.

    Alisema mara kadhaa amekuwa akimpigia simu kaimu katibu wa Yanga, Deosdedit Baraka ili waweze kuzungumza, lakini hajatokea.

    “Nawashangaa sana Yanga maana yule katibu wao mara kadhaa nimempigia simu aje aonane na Mwesigwa ili waweze kupiga hesabu,  lakini hatokei na matokeo yake wanalalamika kwenye vyombo vya habari.”



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: PICHA LINAENDELEA!!TFF YAZUIA MAMILIONI YA YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top