Madrid,Hispania.
KOCHA wa Hispania,Vicente del Bosque,ametangaza kuwa atajiuzulu kibarua hicho hapo Julai 31 baada ya timu hiyo kuvuliwa ubingwa wa Ulaya.
Del Bosque, 65,ambaye tayari alikuwa na mpango huo hata kabla ya Hispania kutupwa nje na Italia katika hatua ya16 siku ya Jumatatu,ameviambia vyombo vya habari vya
AS na Marca jana Alhamis kwamba atajiuzulu kuifundisha La Roja mwishoni mwa mwezi huu pindi mkataba wake utakapokuwa umefikia ukingoni.
Amesema "Bila shaka wala kificho chochote,sina mpango wa kuendelea na wadhifa huu.Hata kama Hispania ingetwaa ubingwa bado uamuzi wangu ungebaki pale pale.Del Bosque,ameiambia RNE Radio.
"Nitaendelea kufanya kazi mpaka Julai 31 pale mkataba wangu utakapokuwa unafikia ukingoni.
Wakati Del Bosque akitangaza uamuzi huo tayari majina ya makocha Joaquin Caparros,Julen Lopetegui na Jose Antonio Camacho yameshaanza kuhusishwa na kuchukua nafasi hiyo.Taarifa kutoka gazeti la Marca zinasema huenda Joaquin Caparros akapewa kibarua hicho kwani ni kipenzi cha Rais wa chama cha soka cha Hispania,Angel Maria Villar.Kocha mpya atatangazwa Julai 19.
Del Bosque aliiwezesha Hispania kutwaa Kombe la dunia mwaka 2010 huko nchini Afrika Kusini kisha ubingwa wa Ulaya (Euro 2012) baada ya kuifunga Italia kwa mabao 4-0 katika mchezo wa fainali.Lakini kombe la dunia la mwaka 2014 halikumuendea vyema,Del Bosque, kwani Hispania ilitolewa katika hatua ya makundi.
0 comments:
Post a Comment