728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, July 01, 2016

    NEYMAR JR AJIFUNGA BARCA MPAKA 2021

    Barcelona, Hispania.

    Neymar Jr ataendelea kuwa Mchezaji na Mali ya Barcelona mpaka mwaka 2021 hii ni baada ya nyota huyo wa zamani wa Santos kukubali mkataba mpya wa miaka mitano wa kuendelea kuitumikia miamba hiyo ya Catalunya.

    Mkataba huyo mpya utamuwezesha,Neymar,24,kuvuna kitita cha €15m ($16m) kama jumla ya mshahara wake wa mwaka na kuvunja uvumi uliozagaa siku za hivi karibuni kuwa staa huyo wa Brazil hakuwa na furaha na hali ya mambo ilivyo Nou Camp na alikuwa akifikiria kuondoka.

    Akithibitisha taarifa hizo kupitia mitandao wake wa Instagram,Neymar,amesema ana furaha isiyo kifani kuendelea kuishi maisha ya ndoto yake ambayo ni kuendelea kuichezea Barcelona.

    Mkataba wa awali wa Neymar na Barcelona ulikuwa unaisha mwaka 2018 hivyo kuongeza miaka mitano zaidi ni kuzima ndoto za vilabu vyote ambavyo vilikuwa vikimuwania staa huyo.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NEYMAR JR AJIFUNGA BARCA MPAKA 2021 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top